Swahili New Testament Bible

Ephesians 5

Ephesians

Return to Index

Chapter 6

1


 

  Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.  

 

 

-

2


 

  "Waheshimu Baba na mama yako," hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,  

 

 

-

3


 

  "Upate fanaka na miaka mingi duniani."  

 

 

-

4


 

  Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.  

 

 

-

5


 

  Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.  

 

 

-

6


 

  Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi ni watumishi wa Kristo.  

 

 

-

7


 

  Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.  

 

 

-

8


 

  Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.  

 

 

-

9


 

  Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, kwake cheo cha mtu si kitu.  

 

 

-

10


 

  Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu.  

 

 

-

11


 

  Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.  

 

 

-

12


 

  Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.  

 

 

-

13


 

  Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti.  

 

 

-

14


 

  Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani,  

 

 

-

15


 

  na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.  

 

 

-

16


 

  Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu.  

 

 

-

17


 

  Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.  

 

 

-

18


 

  Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.  

 

 

-

19


 

  Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti.  

 

 

-

20


 

  Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.  

 

 

-

21


 

  Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.  

 

 

-

22


 

  Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo.  

 

 

-

23


 

  Ninawatakieni ninyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.  

 

 

-

24


 

  Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho.  

 

 

-

Colossians 1

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: