Swahili New Testament Bible

Galatians 4

Galatians

Return to Index

Chapter 5

1


 

  Kristo alitupa uhuru akataka tubaki huru. Basi, simameni imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa.  

 

 

-

2


 

  Sikilizeni! Ni mimi Paulo ninayesema nanyi! Kama mkikubali kutahiriwa, Kristo hatawafaidia chochote.  

 

 

-

3


 

  Nasema tena wazi: kila anayekubali kutahiriwa itambidi kuishika Sheria yote.  

 

 

-

4


 

  Kama mnatazamia kukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Sheria, basi, mmejitenga mbali na Kristo; mko nje ya neema ya Mungu.  

 

 

-

5


 

  Kwa upande wetu, lakini, sisi tunatumaini kwamba kwa nguvu ya Roho tunakubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya imani.  

 

 

-

6


 

  Maana ikiwa tumeungana na Kristo Yesu, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuna maana; cha maana ni imani ifanyayo kazi kwa mapendo. ic  

 

 

-

7


 

  Mwenendo wenu ulikuwa mzuri! Nani, basi aliyewazuia kuuzingatia ukweli?  

 

 

-

8


 

  Aliyesababisha hali hiyo si Mungu ambaye amewaiteni.  

 

 

-

9


 

  "chachu kidogo tu huchachusha donge lote la unga!"  

 

 

-

10


 

  Kutokana na kuungana kwetu na Bwana, nina tumaini kubwa kwamba ninyi hamtakuwa na msimamo tofauti nami. Tena yeyote huyo anayewavurugeni--awe nani au nani--hakika ataadhibiwa.  

 

 

-

11


 

  Na kwa upande wangu, ndugu zangu, kama bado ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini basi, bado ninadhulumiwa? Kama ingalikuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingalileta aibu yoyote.  

 

 

-

12


 

  Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!  

 

 

-

13


 

  Ninyi, ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo.  

 

 

-

14


 

  Maana Sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: "Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."  

 

 

-

15


 

  Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana kama wanyama, jihadharini msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe!  

 

 

-

16


 

  Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia.  

 

 

-

17


 

  Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka ninyi wenyewe.  

 

 

-

18


 

  Kama mkiongozwa na Roho, basi, hamko tena chini ya Sheria.  

 

 

-

19


 

  Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati, ufisadi;  

 

 

-

20


 

  kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano;  

 

 

-

21


 

  husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawatakuwa na nafasi yao katika ufalme wa Mungu.  

 

 

-

22


 

  Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,  

 

 

-

23


 

  upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.  

 

 

-

24


 

  Wale walio wa Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.  

 

 

-

25


 

  Tukiishi kwa msaada wa Roho, na tuufuate mwongozo wake.  

 

 

-

26


 

  Basi, tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu.  

 

 

-

Galatians 6

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: