Swahili New Testament Bible

Acts 10

Acts

Return to Index

Chapter 11

1


 

  Mitume na ndugu kule Yudea walisikia kwamba watu wa mataifa mengine pia walikuwa wamelipokea neno la Mungu.  

 

 

-

2


 

  Basi, Petro aliporudi Yerusalemu, wale Wayahudi waumini waliopendelea watu wa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumu wakisema:  

 

 

-

3


 

  "Wewe umekwenda kukaa na watu wasiotahiriwa na hata umekula pamoja nao!  

 

 

-

4


 

  Hapo Petro akawaeleza kinaganaga juu ya yale yaliyotendeka tangu mwanzo:  

 

 

-

5


 

  "Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa likishushwa chini kutoka mbinguni likiwa limeshikwa pembe zake nne, likawekwa kando yangu.  

 

 

-

6


 

  Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.  

 

 

-

7


 

  Kisha nikasikia sauti ikiniambia: `Petro amka, chinja, ule.`  

 

 

-

8


 

  Lakini mimi nikasema: `La, Bwana; maana chochote kilicho najisi au kichafu hakijapata kamwe kuingia kinywani mwangu.`  

 

 

-

9


 

  Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: `Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa.`  

 

 

-

10


 

  Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni.  

 

 

-

11


 

  Ghafla, watu watatu waliokuwa wametumwa kwangu kutoka Kaisarea waliwasili kwenye nyumba niliyokuwa nakaa.  

 

 

-

12


 

  Roho aliniambia niende pamoja nao bila kusita. Hawa ndugu sita waliandamana nami pia kwenda Kaisarea na huko tuliingia nyumbani mwa Kornelio.  

 

 

-

13


 

  Yeye alitueleza jinsi alivyokuwa amemwona malaika amesimama nyumbani mwake na kumwambia: `Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.  

 

 

-

14


 

  Yeye atakuambia maneno ambayo kwayo wewe na jamaa yako yote mtaokolewa.`  

 

 

-

15


 

  Na nilipoanza tu kuongea, Roho Mtakatifu aliwashukia kama alivyotushukia sisi pale awali.  

 

 

-

16


 

  Hapo nilikumbuka yale maneno Bwana aliyosema: `Yohane alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.`  

 

 

-

17


 

  Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa mataifa mengine zawadi ileile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ni nani hata nijaribu kumpinga Mungu?"  

 

 

-

18


 

  Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, "Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu na kuwa na uzima!"  

 

 

-

19


 

  Kutokana na mateso yaliyotokea wakati Stefano alipouawa, waumini walitawanyika. Wengine walikwenda mpaka Foinike, Kupro na Antiokia wakihubiri ule ujumbe kwa Wayahudi tu.  

 

 

-

20


 

  Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine wakiwahubiria ile Habari Njema juu ya Bwana Yesu.  

 

 

-

21


 

  Bwana aliwasaidia na idadi kubwa ya watu iliamini na kumgeukia Bwana.  

 

 

-

22


 

  Habari ya jambo hilo ikasikika kwa lile kanisa la Yerusalemu. Hivyo wakamtuma Barnaba aende Antiokia.  

 

 

-

23


 

  Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.  

 

 

-

24


 

  Barnaba alikuwa mtu mwema na mwenye kujaa Roho Mtakatifu na imani. Kundi kubwa la watu lilivutwa kwa Bwana.  

 

 

-

25


 

  Kisha, Barnaba alikwenda Tarso kumtafuta Saulo  

 

 

-

26


 

  Alipompata, alimleta Antiokia. Nao wote wawili walikaa na lile kanisa kwa mwaka wote mzima wakifundisha kundi kubwa la watu. Huko Antiokia, ndiko, kwa mara ya kwanza, wafuasi waliitwa Wakristo. ic  

 

 

-

27


 

  Wakati huohuo, manabii kadhaa walikuja Antiokia kutoka Yerusalemu.  

 

 

-

28


 

  Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote (Njaa hiyo ilitokea wakati Klaudio alipokuwa akitawala).  

 

 

-

29


 

  Wale wanafunzi waliamua kila mmoja kwa kadiri ya uwezo wake apeleke chochote ili kuwasaidia wale ndugu waliokuwa wanaishi Yudea.  

 

 

-

30


 

  Basi, wakafanya hivyo na kupeleka mchango wao kwa wazee wa kanisa kwa mikono ya Barnaba na Saulo.  

 

 

-

Acts 12

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: