Swahili New Testament Bible

John 15

John

Return to Index

Chapter 16

1


 

  "Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu.  

 

 

-

2


 

  Watu watawatenga ninyi na masunagogi yao. Tena, wakati unakuja ambapo kila atakayewaua ninyi atadhani anamhudumia Mungu.  

 

 

-

3


 

  Watawatendeeni mambo hayo kwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi.  

 

 

-

4


 

  Basi, nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika mkumbuke kwamba niliwaambieni. "Sikuwaambieni mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.  

 

 

-

5


 

  Lakini sasa namwendea yule aliyenituma; na hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: `Unakwenda wapi?`  

 

 

-

6


 

  Kwa kuwa nimewaambieni mambo hayo mmejaa huzuni mioyoni mwenu.  

 

 

-

7


 

  Lakini, nawaambieni ukweli: afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu.  

 

 

-

8


 

  Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu.  

 

 

-

9


 

  Wamekosea kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini;  

 

 

-

10


 

  kuhusu uadilifu, kwa sababu naenda zangu kwa Baba, nanyi hamtaniona tena;  

 

 

-

11


 

  kuhusu hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa.  

 

 

-

12


 

  "Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili.  

 

 

-

13


 

  Lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atawaambieni yote atakayosikia, na atasema mambo yatakayokuwa yanakuja.  

 

 

-

14


 

  Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.  

 

 

-

15


 

  Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu; ndiyo maana nimesema kwamba huyo Roho Mtakatifu atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.  

 

 

-

16


 

  "Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!"  

 

 

-

17


 

  Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, "Ana maana gani anapotwambia: `Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?` Tena anasema: `Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!"`  

 

 

-

18


 

  Basi, wakawa wanaulizana, "Ana maana gani anaposema: `Bado kitambo kidogo?` Hatuelewi anaongelea nini."  

 

 

-

19


 

  Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, "Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: `Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?`  

 

 

-

20


 

  Nawaambieni kweli, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi: mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.  

 

 

-

21


 

  Wakati mama anapojifungua huona huzuni kwa sababu saa ya maumivu imefika; lakini akisha jifungua hayakumbuki tena maumivu hayo kwa sababu ya furaha kwamba mtu amezaliwa duniani.  

 

 

-

22


 

  Ninyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.  

 

 

-

23


 

  Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni.  

 

 

-

24


 

  Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.  

 

 

-

25


 

  "Nimewaambieni mambo hayo kwa mafumbo. Lakini wakati utakuja ambapo sitasema tena nanyi kwa mafumbo, bali nitawaambieni waziwazi juu ya Baba.  

 

 

-

26


 

  Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;  

 

 

-

27


 

  maana yeye mwenyewe anawapenda ninyi, kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu.  

 

 

-

28


 

  Mimi nilitoka kwa Baba, nikaja ulimwenguni; na sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwa Baba."  

 

 

-

29


 

  Basi, wanafunzi wake wakamwambia, "Ahaa! Sasa unasema waziwazi kabisa bila kutumia mafumbo.  

 

 

-

30


 

  Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu."  

 

 

-

31


 

  Yesu akawajibu, "Je, mnaamini sasa?  

 

 

-

32


 

  Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo ninyi nyote mtatawanyika kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami.  

 

 

-

33


 

  Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!"  

 

 

-

John 17

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: