Swahili New Testament Bible

John 11

John

Return to Index

Chapter 12

1


 

  Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alifika Bethania alikoishi Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua kutoka wafu.  

 

 

-

2


 

  Huko walimwandalia chakula cha jioni, naye Martha akawa anawatumikia. Lazaro alikuwa mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja na Yesu.  

 

 

-

3


 

  Basi, Maria alichukua chupa ya marashi ya nardo safi ya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu ya marashi.  

 

 

-

4


 

  Basi, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,  

 

 

-

5


 

  "Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha dinari mia tatu, wakapewa maskini?"  

 

 

-

6


 

  Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina.  

 

 

-

7


 

  Lakini Yesu akasema, "Msimsumbue huyu mama! Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishi yangu.  

 

 

-

8


 

  Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote." ic  

 

 

-

9


 

  Wayahudi wengi walisikia kwamba Yesu alikuwa Bethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajili ya kumwona Yesu, ila pia wapate kumwona Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka wafu.  

 

 

-

10


 

  Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro,  

 

 

-

11


 

  Maana kwa sababu ya Lazaro Wayahudi wengi waliwaasi viongozi wao, wakamwamini Yesu.  

 

 

-

12


 

  Kesho yake, kundi kubwa la watu waliokuja kwenye sikukuu walisikia kuwa Yesu alikuwa njiani kuja Yerusalemu.  

 

 

-

13


 

  Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaaza sauti wakisema: "Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana. Abarikiwe mfalme wa Israeli."  

 

 

-

14


 

  Yesu akampata mwana punda mmoja akapanda juu yake kama yasemavyo Maandiko:  

 

 

-

15


 

  "Usiogope mji wa Sioni! Tazama, Mfalme wako anakuja, Amepanda mwana punda."  

 

 

-

16


 

  Wakati huo wanafunzi wake hawakuelewa mambo hayo, lakini Yesu alipokwisha tukuzwa, ndipo walipokumbuka kwamba hayo yalikuwa yameandikwa juu yake, na kwamba watu walikuwa wamemtendea hivyo.  

 

 

-

17


 

  Kundi la watu wale waliokuwa pamoja naye wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka wafu, walisema yaliyotukia.  

 

 

-

18


 

  Kwa hiyo umati huo wa watu ulimlaki, maana wote walisikia kwamba Yesu alikuwa amefanya ishara hiyo.  

 

 

-

19


 

  Basi, Mafarisayo wakaambiana, "Mnaona? Hatuwezi kufanya chochote! Tazameni, ulimwengu wote unamfuata."  

 

 

-

20


 

  Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo.  

 

 

-

21


 

  Hao walimwendea Filipo, mwenyeji wa Bethsaida katika Galilaya, wakasema, "Mheshimiwa, tunataka kumwona Yesu."  

 

 

-

22


 

  Filipo akaenda akamwambia Andrea, nao wawili wakaenda kumwambia Yesu.  

 

 

-

23


 

  Yesu akawaambia, "Saa ya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtu imefika!  

 

 

-

24


 

  Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubaki punje tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa. Kama ikifa, basi huzaa matunda mengi.  

 

 

-

25


 

  Anayependa maisha yake, atayapoteza; anayeyachukia maisha yake katika ulimwengu huu, atayaweka kwa ajili ya uzima wa milele.  

 

 

-

26


 

  Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate, hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikia Baba yangu atampa heshima.  

 

 

-

27


 

  "Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: `Baba, usiruhusu saa hii inifikie`? Lakini ndiyo maana nimekuja--ili nipite katika saa hii.  

 

 

-

28


 

  Baba, ulitukuze jina lako." Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, "Nimelitukuza, na nitalitukuza tena."  

 

 

-

29


 

  Umati wa watu waliokuwa wamesimama hapo walisikia sauti hiyo, na baadhi yao walisema, "Malaika ameongea naye!"  

 

 

-

30


 

  Lakini Yesu akawaambia, "Sauti hiyo haikutokea kwa ajili yangu mimi, ila kwa ajili yenu.  

 

 

-

31


 

  Sasa ndio wakati wa ulimwengu huu kuhukumiwa; sasa mtawala wa ulimwengu huu atapinduliwa.  

 

 

-

32


 

  Nami nitakapoinuliwa juu ya nchi nitamvuta kila mmoja kwangu."  

 

 

-

33


 

  Kwa kusema hivyo alionyesha atakufa kifo gani).  

 

 

-

34


 

  Basi, umati huo ukamjibu, "Sisi tunaambiwa na Sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?"  

 

 

-

35


 

  Yesu akawaambia, "Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.  

 

 

-

36


 

  Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga." Baada ya kusema maneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao.  

 

 

-

37


 

  Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini.  

 

 

-

38


 

  Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia: "Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu? Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?"  

 

 

-

39


 

  Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya tena alisema:  

 

 

-

40


 

  "Mungu ameyapofusha macho yao, amezipumbaza akili zao; wasione kwa macho yao, wasielewe kwa akili zao; wala wasinigeukie, asema Bwana, ili nipate kuwaponya."  

 

 

-

41


 

  Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.  

 

 

-

42


 

  Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi.  

 

 

-

43


 

  Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu  

 

 

-

44


 

  Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, "Mtu aliyeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma.  

 

 

-

45


 

  Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma.  

 

 

-

46


 

  Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani.  

 

 

-

47


 

  Anayeyasikia maneno yangu lakini hayashiki mimi sitamhukumu; maana sikuja kuhukumu ulimwengu bali kuuokoa.  

 

 

-

48


 

  Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho.  

 

 

-

49


 

  Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini.  

 

 

-

50


 

  Nami najua kuwa amri yake huleta uzima wa milele. Basi, mimi nasema tu yale Baba aliyoniagiza niyaseme."  

 

 

-

John 13

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: