Swahili New Testament Bible

John 10

John

Return to Index

Chapter 11

1


 

  Mtu mmoja aitwaye Lazaro, mwenyeji wa Bethania, alikuwa mgonjwa. (Kijiji cha Bethania kilikuwa mahali walipokaa Maria na Martha, dada yake.  

 

 

-

2


 

  Maria ndiye yule aliyempaka Bwana marashi na kumpangusa kwa nywele zake. Lazaro, kaka yake, ndiye aliyekuwa mgonjwa.)  

 

 

-

3


 

  Basi, hao dada wakatuma ujumbe huu kwa Yesu: "Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!"  

 

 

-

4


 

  Yesu aliposikia hivyo akasema, "Ugonjwa huo hautaleta kifo, ila ni kwa ajili ya kumtukuza Mungu; ameugua ili kwa njia hiyo Mwana wa Mungu atukuzwe."  

 

 

-

5


 

  Yesu aliwapenda Martha, dada yake na Lazaro.  

 

 

-

6


 

  Alipopata habari kwamba Lazaro ni mgonjwa, Yesu aliendelea kukaa mahali hapo alipokuwa kwa siku mbili zaidi.  

 

 

-

7


 

  Kisha akawaambia wanafunzi wake, "Twendeni tena Yudea!"  

 

 

-

8


 

  Wanafunzi wakamwambia, "Mwalimu! Muda mfupi tu umepita tangu Wayahudi walipotaka kukuua kwa mawe, nawe unataka kwenda huko tena?"  

 

 

-

9


 

  Yesu akajibu, "Je, saa za mchana si kumi na mbili? Basi, mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa kuwa anauona mwanga wa ulimwengu huu.  

 

 

-

10


 

  Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maana mwanga haumo ndani yake."  

 

 

-

11


 

  Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, akawaambia, "Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini mimi nitakwenda kumwamsha."  

 

 

-

12


 

  Wanafunzi wake wakamwambia, "Bwana, ikiwa amelala, basi atapona."  

 

 

-

13


 

  Wao walidhani kwamba alikuwa amesema juu ya kulala usingizi, kumbe alikuwa amesema juu ya kifo cha Lazaro.  

 

 

-

14


 

  Basi, Yesu akawaambia waziwazi, "Lazaro amekufa;  

 

 

-

15


 

  Lakini nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini. Haya, twendeni kwake."  

 

 

-

16


 

  Thoma (aitwaye Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, "Twendeni nasi tukafe pamoja naye!"  

 

 

-

17


 

  Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne.  

 

 

-

18


 

  Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu umbali upatao kilomita tatu.  

 

 

-

19


 

  Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao.  

 

 

-

20


 

  Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani.  

 

 

-

21


 

  Martha akamwambia Yesu, "Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!  

 

 

-

22


 

  Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa."  

 

 

-

23


 

  Yesu akamwambia, "Kaka yako atafufuka."  

 

 

-

24


 

  Martha akamjibu, "Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho."  

 

 

-

25


 

  Yesu akamwambia, "Mimi ndimi ufufuo na uzima. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi:  

 

 

-

26


 

  na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?"  

 

 

-

27


 

  Martha akamwambia, "Ndiyo Bwana! Naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni."  

 

 

-

28


 

  Baada ya kusema hayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwabia faraghani, "Mwalimu yuko hapa, anakuita."  

 

 

-

29


 

  Naye aliposikia hivyo, akainuka mara, akamwendea Yesu.  

 

 

-

30


 

  Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado mahali palepale Martha alipomlaki.  

 

 

-

31


 

  Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.  

 

 

-

32


 

  Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwabia, "Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!"  

 

 

-

33


 

  Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni.  

 

 

-

34


 

  Kisha akawauliza, "Mlimweka wapi?" Wakamwambia, "Bwana, njoo uone."  

 

 

-

35


 

  Yesu akalia machozi.  

 

 

-

36


 

  Basi, Wayahudi wakasema, "Tazameni jinsi alivyompenda!"  

 

 

-

37


 

  Lakini baadhi yao wakasema, "Je, huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya Lazaro asife?"  

 

 

-

38


 

  Basi, Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni, akafika kaburini. Kaburi lenyewe lilikuwa pango, na lilikuwa limefunikwa kwa jiwe.  

 

 

-

39


 

  Yesu akasema, "Ondoeni hilo jiwe!" Martha, dada yake huyo aliyekufa, akamwambia, "Bwana, amekwishaanza kunuka; amekaa kaburini siku nne!"  

 

 

-

40


 

  Yesu akamwambia, "Je, sikukwambia kwamba ukiamini utaona utukufu wa Mungu?"  

 

 

-

41


 

  Basi, wakaliondoa lile jiwe. Yesu akatazama juu mbinguni, akasema, "Nakushukuru Baba kwa kuwa wewe wanisikiliza.  

 

 

-

42


 

  Najua kwamba unanisikiliza daima. Lakini nimesema hayo kwa ajili ya watu hawa waliopo hapa ili wapate kuamini kwamba wewe ndiwe uliyenituma."  

 

 

-

43


 

  Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: "Lazaro! Toka nje!"  

 

 

-

44


 

  Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, "Mfungueni, mkamwache aende zake."  

 

 

-

45


 

  Basi, Wayahudi wengi waliokuwa wamefika kwa Maria walipoona kitendo hicho alichokifanya Yesu wakamwamini.  

 

 

-

46


 

  Lakini baadhi yao walikwenda kwa Mafarisayo wakatoa taarifa ya jambo hilo alilofanya Yesu.  

 

 

-

47


 

  kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza kuu, wakasema, "Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno.  

 

 

-

48


 

  Tukimwacha tu watu wote watamwamini, nao Waroma watakuja kuliharibu Hekalu letu na taifa letu!"  

 

 

-

49


 

  Hapo, mmoja wao aitwaye Kayafa, ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, akawaambia, "Ninyi hamjui kitu!  

 

 

-

50


 

  Je, hamwoni kwamba ni afadhali kwenu mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa zima liangamizwe?"  

 

 

-

51


 

  Yeye hakusema hivyo kwa hiari yake mwenyewe, bali kwa vile alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, alibashiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa lao;  

 

 

-

52


 

  na wala si kwa ajili yao tu, bali pia apate kuwaleta pamoja watoto wa Mungu waliotawanyika.  

 

 

-

53


 

  Basi, tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi walifanya mipango ya kumwua Yesu.  

 

 

-

54


 

  Kwa hiyo, Yesu hakutembea tena hadharani kati ya Wayahudi, bali alitoka hapo, akaenda mahali karibu na jangwa, katika mji uitwao Efraimu. Akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.  

 

 

-

55


 

  Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa karibu, na watu wengi walikwenda Yerusalemu ili wajitakase kabla ya sikukuu hiyo.  

 

 

-

56


 

  Basi, wakawa wanamtafuta Yesu; nao walipokusanyika pamoja Hekaluni wakaulizana, "Mwaonaje? Yaonekana kwamba haji kabisa kwenye sikukuu, au sivyo?"  

 

 

-

57


 

  Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba mtu akijua mahali aliko Yesu awaarifu kusudi wamtie nguvuni.  

 

 

-

John 12

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: