Swahili New Testament Bible

Luke 18

Luke

Return to Index

Chapter 19

1


 

  Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo.  

 

 

-

2


 

  Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.  

 

 

-

3


 

  Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu.  

 

 

-

4


 

  Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo.  

 

 

-

5


 

  Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, "Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako."  

 

 

-

6


 

  Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.  

 

 

-

7


 

  Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunung`unika wakisema, "Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi."  

 

 

-

8


 

  Lakini Zakayo akasimama akamwambia Yesu, "Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyang`anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne."  

 

 

-

9


 

  Yesu akamwambia, "Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.  

 

 

-

10


 

  Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea." ic  

 

 

-

11


 

  Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. (Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, Ufalme wa Mungu ungefika.)  

 

 

-

12


 

  Hivyo akawaambia, "Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.  

 

 

-

13


 

  Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kumwambia: `Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.`  

 

 

-

14


 

  Lakini wananchi wenzake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende wakaseme: `Hatumtaki huyu atutawale.`  

 

 

-

15


 

  "Huyo mtu mashuhuri alirudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, na mara akaamuru wale watumishi aliowapa zile fedha waitwe ili aweze kujua kila mmoja amepata faida gani.  

 

 

-

16


 

  Mtumishi wa kwanza akatokea, akasema: `Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara kumi ya zile fedha ulizonipa.`  

 

 

-

17


 

  Naye akamwambia: `Vema; wewe ni mtumishi mwema. Kwa kuwa umekuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi!`  

 

 

-

18


 

  Mtumishi wa pili akaja, akasema: `Mheshimiwa, faida iliyopatikana ni mara tano ya zile fedha ulizonipa.`  

 

 

-

19


 

  Naye akamwambia pia: `Nawe utakuwa na madaraka juu ya miji mitano.`  

 

 

-

20


 

  "Mtumishi mwingine akaja, akasema: `Chukua fedha yako; niliificha salama katika kitambaa,  

 

 

-

21


 

  kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na huchuma ambacho hukupanda.`  

 

 

-

22


 

  Naye akamwambia: `Nakuhukumu kutokana na msemo wako, ewe mtumishi mbaya! Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, ambaye huchukua yasiyo yangu na kuchuma nisichopanda.  

 

 

-

23


 

  Kwa nini basi, hukuiweka fedha yangu benki, nami ningeichukua pamoja na faida baada ya kurudi kwangu?`  

 

 

-

24


 

  Hapo akawaambia wale waliokuwa pale: `Mnyang`anyeni hizo fedha, mkampe yule aliyepata faida mara kumi.`  

 

 

-

25


 

  Nao wakamwambia: `Lakini Mheshimiwa, huyo ana faida ya kiasi hicho mara kumi!`  

 

 

-

26


 

  Naye akawajibu: `Kila aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.  

 

 

-

27


 

  Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu."`  

 

 

-

28


 

  Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu.  

 

 

-

29


 

  Alipokaribia kufika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,  

 

 

-

30


 

  akawaambia: "Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana punda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamlete hapa.  

 

 

-

31


 

  Kama mtu akiwauliza, kwa nini mnamfungua, mwambieni, `Bwana ana haja naye."`  

 

 

-

32


 

  Basi, wakaenda, wakakuta sawa kama alivyowaambia.  

 

 

-

33


 

  Walipokuwa wanamfungua yule mwana punda, wenyewe wakawauliza, "Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?"  

 

 

-

34


 

  Nao wakawajibu, "Bwana anamhitaji."  

 

 

-

35


 

  Basi, wakampelekea Yesu yule mwana punda. Kisha wakatandika mavazi yao juu yake wakampandisha Yesu.  

 

 

-

36


 

  Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani.  

 

 

-

37


 

  Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake, wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;  

 

 

-

38


 

  wakawa wanasema: "Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!"  

 

 

-

39


 

  Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu, wakamwambia Yesu, "Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!"  

 

 

-

40


 

  Yesu akawajibu, "Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti."  

 

 

-

41


 

  Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia  

 

 

-

42


 

  akisema: "Laiti ungelijua leo hii yale yaletayo amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.  

 

 

-

43


 

  Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote.  

 

 

-

44


 

  Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hata jiwe moja juu jingine, kwa sababu hukuutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa."  

 

 

-

45


 

  Kisha, Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuzia nje wafanyabiashara  

 

 

-

46


 

  akisema, "Imeandikwa: `Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala`; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang`anyi."  

 

 

-

47


 

  Yesu akawa anafundisha kila siku Hekaluni. Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumwangamiza,  

 

 

-

48


 

  lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa.  

 

 

-

Luke 20

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: