Swahili New Testament Bible

Mark 2

Mark

Return to Index

Chapter 3

1


 

  Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza.  

 

 

-

2


 

  Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki.  

 

 

-

3


 

  Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, "Njoo hapa katikati."  

 

 

-

4


 

  Kisha, akawauliza, "Je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuua?" Lakini wao hawakusema neno.  

 

 

-

5


 

  Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia huyo mtu, "Nyosha mkono wako!" Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.  

 

 

-

6


 

  Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wa kikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu.  

 

 

-

7


 

  Yesu aliondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaenda kando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea,  

 

 

-

8


 

  Idumea, ng`ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.  

 

 

-

9


 

  Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.  

 

 

-

10


 

  Alikuwa amewaponya watu wengi, na wagonjwa wote wakawa wanamsonga ili wapate kumgusa.  

 

 

-

11


 

  Na watu waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake na kupaaza sauti, "Wewe ni Mwana wa Mungu!"  

 

 

-

12


 

  Lakini Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu.  

 

 

-

13


 

  Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea,  

 

 

-

14


 

  naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume,*fb* wakae naye, awatume kuhubiri  

 

 

-

15


 

  na wawe na mamlaka ya kuwafukuza pepo.  

 

 

-

16


 

  Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro),  

 

 

-

17


 

  Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake "wanangurumo"),  

 

 

-

18


 

  Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani na  

 

 

-

19


 

  Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.  

 

 

-

20


 

  Kisha Yesu alikwenda nyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula.  

 

 

-

21


 

  Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo wakatoka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasema kwamba amepatwa na wazimu.  

 

 

-

22


 

  Nao walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, "Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo."  

 

 

-

23


 

  Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwa mifano,"Shetani anawezaje kumfukuza Shetani?  

 

 

-

24


 

  Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopigana, utawala huo hauwezi kudumu.  

 

 

-

25


 

  Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia.  

 

 

-

26


 

  Ikiwa basi, utawala wa Shetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu, bali utaangamia kabisa.  

 

 

-

27


 

  "Hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang`anya mali yake, isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kumnyang`anya mali yake.  

 

 

-

28


 

  "Kweli nawaambieni, watu watasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote;  

 

 

-

29


 

  lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele."  

 

 

-

30


 

  Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema, "Ana pepo mchafu.")  

 

 

-

31


 

  Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekea ujumbe kutaka kumwona.  

 

 

-

32


 

  Umati wa watu ulikuwa umekaa hapo kumzunguka. Basi, wakamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona."  

 

 

-

33


 

  Yesu akawaambia, "Mama yangu na ndugu zangu ni kina nani?"  

 

 

-

34


 

  Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema, "Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu.  

 

 

-

35


 

  Mtu yeyote anayefanya anayotaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu."  

 

 

-

Mark 4

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: