Swahili New Testament Bible

Matthew 3

Matthew

Return to Index

Chapter 4

1


 

  Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.  

 

 

-

2


 

  Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.  

 

 

-

3


 

  Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate."  

 

 

-

4


 

  Yesu akamjibu, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: `Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu."`  

 

 

-

5


 

  Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,  

 

 

-

6


 

  akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: `Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe."`  

 

 

-

7


 

  Yesu akamwambia, "Imeandikwa pia: `Usimjaribu Bwana, Mungu wako."`  

 

 

-

8


 

  Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,  

 

 

-

9


 

  akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu."  

 

 

-

10


 

  Hapo, Yesu akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake."`  

 

 

-

11


 

  Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.  

 

 

-

12


 

  Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.  

 

 

-

13


 

  Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.  

 

 

-

14


 

  Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:  

 

 

-

15


 

  "Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng`ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!  

 

 

-

16


 

  Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!"  

 

 

-

17


 

  Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, "Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!"  

 

 

-

18


 

  Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.  

 

 

-

19


 

  Basi, akawaambia, "Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."  

 

 

-

20


 

  Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. ic  

 

 

-

21


 

  Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita,  

 

 

-

22


 

  nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.  

 

 

-

23


 

  Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.  

 

 

-

24


 

  Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.  

 

 

-

25


 

  Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng`ambo ya mto Yordani, walimfuata.  

 

 

-

Matthew 5

 

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: